Uganda:
Mishahara ya Polisi wa Uganda imechelewa kuwafikia askari polisi wa nchi hiyo kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika mapema, imeripotiwa.
Kucheleweshwa huko kwa mishahara kumepelekea mihangaiko kwa baadhi ya maofisa polisi waliohitaji kulipa mikopo yao na wengine hata kushindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni, imeripotiwa.
“Our salaries haven’t been sent to our accounts but the officers should be patient.” Deputy Police Spokesperson Patrick Onyango confirmed
Onyango, aliongeza kuwa tatizo hilo si askari polisi pekeyake ambao hawajalipwa mishahara hiyo mpaka bali pia imeathiri sehemu nyingine kama maafisa magereza, walimu na hata madaktari.
Mr Jonas Tumwine akiongea kwa niaba ya wizara amesema tatizo hilo limetokana na upungufu wa fedha ( shortage of funds ).
“We have had meetings with the affected ministries and they are aware of what is happening. We have also filed for a supplementary budget to the Finance ministry,”
first posted on June11/2013