Makamu wa Raisi wa Kenya William Ruto alazimika kwenda the Hague
Mahakama ya kimataifa inayo shughurikia kesi za waharifu wa kimataifa (The Hague) leo ilifanya mkutano kuangalia makubaliano ya ni jinsi gani ya kuendelea na hukumu ya kesi inayo wahusisha viongozi wa serikali ya Kenya ikiwa ni pamoja na Makamu wa raisi wa Kenya William Ruto na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang.
Mh: Ruto ambaye mapema aliwaomba Majaji wa mahakama hiyo ya kimataifa kuweza kumruhusu kumkubalia kushiriki katika usikilizaji wa kesi hiyo kwa njia ya kupitia mawasiliano ya video yaani (via video link), lakini alilazimika kusafiri kwenda the hague siku ya jumatatu baada ya mahakimu kutupilia mbali maombi yake.
Kesi hiyo inayo wahusu Ruto na Sang ilipangwa kuanza 28th
may, lakini imesimamishwa baada ya Ruto kupitia wakili Karim Khan kuiomba mahakama kuisogeza mbele mpaka November ili kutoa muda mzuri wa maandalizi baada ya wakili kushindwa kuwakilisha ushahidi japokua alitakiwa kufanya hivyo na majaji.