Wanamgodi 264 South Afrika wafunguliwa shtaka la mauaji,

Baadhi ya wafanyakazi waliokamatwa Afrika ya Kusini katika mgomo wa wafanyakazi katika mgodi wa Marikana wameshtakiwa na kosa la mauji ya wafanyakazi wenzao 34 waliopigwa risasi na Polisi. 
Wafanyakazi hao wapatao 270 watahukumiwa chini ya kanuni ya kawaida kwa kupambana na polisi kati ya tarehe 16 mwezi wa nane.
Kiongozi wa zamani wa vijana wa chama cha ANC Julius Malema amekaririwa akisema maamuzi hayo ya kimahakama si sawa, akihoji kwanini Polisi hata mmoja kati yao hajawekwa chini vyombo vya sheria.
Malema akisisitiza juu ya tukio hilo kuonekana na Dunia nzima amesema anaangalia uwezekano juu ya kuwataka mawakili wa ulinzi kufanya maombi ya haraka kuwakilisha madai hayo katika mahakama kuu.
Wafanyakazi 264 ndio waliofikishwa mahakamani hapo karibu na mji wa Pretoria, ambapo 6 kati yao bado wapo hospitalini kutokana na majeraha waliyo yapata katika tukio hilo ambalo lilipoteza maisha ya wafanyakazi wapatao 34.

Strange/Ajabu

Sports/michezo

Hotpost