Hospitali ya taifa ya nchini Kenya, (KENYATTA National Hospital) wamekata rufaa kwa serikali kwa kuitaka iharakishe tamko kuhusu madaktari kusitisha mgomo wao unao endelea.
Mgomo ambao umekuwepo kwa muda wa siku kadhaa sasa uliitishwa na Kenya Medical Pharmacists na chama cha madaktari wa meno kuitaka serikali kuanzisha mfumo wa kurudi kazini ambao umetokea kutokana na msimamo wa viwanda mwaka uliopita.
CEO Richard Lesiyampe katika mazungumzo yake ametaka kushughulikiwa haraka kwa masuala ya msingi yaliyojitokeza kabla wananchi na wagonjwa hawajapatwa na madhara zaidi kutokana na tatizo hilo, akisisitiza ya kua mpaka sasa hospitali imeshapata madhara makubwa kutokana na mgomo huo.
