Waziri Mkuu wa Kenya awatakawawekezaji nchini humo kuwekeza zaidi katika kipindi hiki


Kenya:
Waziri Mkuu wa Kenya mh Raila Odinga amewataka wawekezaji wa kigeni kutafuta nafasi za kuwekeza zaidi katika fursa za kibiashara nchini humo katika kipindi hiki.

Odinga amekaririwa akiyasema hayo siku ya Jumanne katika kusheherekea miaka 22 ya muungano wa Ujerumani.
Akikazia kwa kuwepo kwa amani ya kutosha katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyia nchini humo Waziri Mkuu huyo alielezea kuwepo kwa uhuru na usawa katika uchaguzi huo.

"Nina watakeni kwa yeyote anaye hitaji kuwekeza katika nchi afanye hivyo wakati huu kwani akichelewa mpaka wakati wa uchaguzi atakua amechelewa sana kwani atakuwa akishindana na wengine wengi katika nafasi hizo," aliendelea kwa kufafanua kwamba nchi ya Kenya imeshapata uzoefu kupitia machfuko yaliyotokea mwaka 2008 na kwamba nchi hiyo haita chagua tena kupitia njia ya machafuko.

Katika kumalizia waziri Mkuu alisisitiza Kenya na Germany kuendelea kukuza biashara na mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Strange/Ajabu

Sports/michezo

Hotpost