Tanzania imewasimamisha wakuu wa idala wanyamapori kwa tuhuma za kusafirisha nje ya nchi wanyamapori pamoja na ndege zaidi ya mia moja kinyume na sheria, imeripotiwa.
Wakuu hao akiwemo Obeid Mbwagwa director wameshutumiwa kuhusika na uhamishaji wanyama kuelekea Qatar kwa kutumia ndege ya kijeshi kati ya mwezi wa 11, 2010. Hata hivyo tayari walishapewa barua za kusimama kazi kwa mujibu taarifa ya waziri wa Maliasilina Utalii Hamisi Kagasheki.
Kagasheki amesema uchunguzi ukonjiani na jopo la wachunguzi litasafiri kuelekea Qatar kwa ajili ya mahojiano na Rubani wa ndege hiyo, pia jopo hilo litakua na kazi ya kuhakiki vibali vilivyotumika na kujionea macho wanyama hao.